29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya Canara yasaidia madawati 100 Kisutu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Benki ya Canara imetoa msaada wa madawati 100 katika Shule ya Msingi Kisutu ili kuboresha utoaji elimu katika shule hiyo.

Msaada huo ambao ulipokelewa na Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora Tenga, ni mwendelezo wa sera ya benki hiyo kuchangia huduma za jamii kukabili changamoto zilizoko katika sekta mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Canara Tanzania, Balaji Rao, akikabidhi madawati kwa Ofisa Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora Tenga. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisutu, Elizabeth Massawe na (Wapili Kulia) ni Ofisa Elimu Kata ya Kisutu, Renalda Macha. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya shule hiyo.

Akipokea msaada huo Sipora amesema wanatambua na kuthamini mchango wa benki hiyo na kwamba msaada huo utaongeza chachu kwa watoto kupata elimu katika mazingira bora.

Amesema Jiji la Dar es Salaam lina wanafunzi wengi na kuwaomba wadau wengine kuendelea kulisaidia ili watoto waweze kusoma vizuri.

“Napenda kutoa shukrani zangu kwa Benki ya Canara kwa jinsi ambavyo imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto zilizoko kwenye sekta ya elimu,” amesema Sipora.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Elizabeth Massawe, amesema msaada huo utasaidia kupunguza upungufu wa madawati katika shule hiyo na kuwawezesha wanafunzi 300 kukaa watatu watatu badala ya wanne kama ilivyokuwa awali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Canara Tanzania, Balaji Rao, amesema ni utaratibu wa benki hiyo kurudisha kwa jamii sehemu ya faida wanayopata kwa sababu jamii ndiyo wanayoihudumia.

“Sisi kama wadau wa maendeleo tuna wajibu wa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kusaidia jamii kwani ndiyo imeifanya benki yetu kuwa hapa ilipo, tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayotuzunguka,” amesema Rao

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles