29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yawataka wafanyabiashara wa madini Mwanza kuhamia soko jipya

Yatoa onyo kwa watakaokaidi kutopewa leseni

Na Clara Matimo, Mwanza

Serikali imewataka  wafanyabiashara wa madini Mkoani Mwanza walio na ofisi katika jengo la Rock City Mall,  kuhamia kwenye soko jipya la madini lililopo Kata ya pasiansi  Wilaya ya Ilemela kilipo kiwanda cha kusafisha dhahabu Mwanza Precious Metal Refinery.

Pia imesema baada ya kukamilisha usajili wa viwanda vya kusafisha dhahabu vilivyopo mikoa ya Mwanza, Geita na Dodoma itazuia usafirishaji wa dhahabu ambayo haijasafishwa kwenda nje ya nchi.

Agizo hilo limetolewa Oktoba 11, jijini hapa na Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko, wakati akizungumza na wafanyabiashara pamoja na wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Mwanza ili kubaini changamoto zao.

Alisema wafanyabiashara watakaokaidi kuhamia katika soko hilo wizara hiyo haitashughulika na maombi yao ya leseni ambazo zimekwisha muda wake  kwa kuwa serikali imetumia gharama kubwa kuhakikisha ujenzi wa soko hilo unakamilika lengo likiwa ni kuwawekea mazingira bor na rafiki.

“ Mimi ninauwezo wa kusema muhame ndani ya wiki mbili zijazo  lakini sitaki kuonekana dikteta, dealers wote simameni niwaone ambaye anasema yeye hawezi kwenda kwenye hilo soko  jipya aniambie hapa hapa ili tusihangaishane na maombi yake ya leseni tutamtafutia eneo lingine aende.

“Nyie wenyewe mliniambia moja ya changamoto ni gharama kubwa hapo rock city mall mnalipa Sh milioni tano hadi tisa kwa mwaka , nia ya serikali ni  kuwatua mzigo huko tunakowapeleka ni jengo la serikali  mtalipa umeme na maji tu hamtalipa gharama zingine zozote na mazingira ni rafiki mnataka tuwafanyie nini?Alihoji ” Biteko.

Alisema nia ya serikali ni kuona wachimbaji madini wanafanya shughuli zao kwa uhuru bila kuonewa wala kunyanyaswa na wao walipe kodi stahiki ndiyo maana iko mstali wa mbele kuwatatulia changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.

Akizungumzia kuzuia kusafirisha nje dhahabu ambayo haijasafishwa, Waziri Biteko alisema “Tukikamilisha usajili  yaani certification tutasafirisha  tu nje ya nchi dhahabu ambayo imeishasafishwa  kwa sababu mimi nitakuwa waziri wa ajabu sana nina feed refinery za wengine halafu tuna refinery humu ndani ambazo sisi wenyewe tumevutia mitaji watu wamewekeza halafu hawapati malighafi,”alisema.

Awali akisoma hotuba  ya wachimbaji mbele ya Waziri Biteko, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Mwanza (Mwarema) Richard Seni, alitaja miongoni mwa changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na ukubwa wa tozo za halamshauri ambazo zinazidi mrabaha na zinatozwa kwenye malighafi ambapo alipendekeza kuondolewa tozo zote zinazokinzana na sheria ya madini ibaki asilimia 0.3 pekee ambayo nayo itozwe kwenye madini.

Vile vile aliiomba serikali maeneo yote ya rush yapatiwe leseni yakiwemo Ghatta Mining Group, Mlimani Mining Group lengo ni kupunguza migogoro lakini pia kuwafanya wachimbaji kuwekeza mitaji yao kwa uhuru na uhakika kitendo kitakachowafanya kukopesheka kwa urahisi zaidi.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dk. Angeline Mabula, alisema uwepo wa kiwanda hicho jimboni humo  kimewezesha kutoa ajira kwa vijana inayowawezesha kujikimu kimaisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles