22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

BENKI YA WANAWAKE, TPB ZAUNGANA

|Mwandishi Wetu, Dar es SalaamBenki ya Wanawake (TWB) imeungana na Benki ya TPB baada ya benki hiyo kushindwa kutimiza masharti ya kuwa na mtaji wa kutosha kujiendesha.

Kutokana na hatua hiyo, wateja, wafanyakazi, mali na madeni yote ya TWB yataunganishwa na Benki ya TPB kuanzia leo.

Hayo yamesemwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Agosti 2, kuhusu hatua mbalimbali benki hiyo ilizochukua kwa baadhi ya benki ambazo zimekiuka masharti ya Sheria ya mabenki na taasisi za fedha.

Amesema Januari 4, mwaka huu iliziongezea  muda wa miezi sita benki nne za Tandahimba Community Bank (Tacoba), Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) na Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) hadi Juni 30, mwaka huu ili kufanikisha kiwango cha mtaji kinachohitajika na sheria za mabenki  na kanuni zake cha kiwango cha chini cha mtaji wa Sh bilioni mbili kwa benki.

Aidha, amesema hata baada ya muda huo kuisha na kuongezewa mwezi mmoja hadi Julai 31, mwaka huu ili kukamilisha benki mtaji, benki mbili zilifanikiwa huku TWB ikishindwa.

Ameanisha Benki ya Tacoba na KCBL kwa sasa zimeongeza mtaji na kukidhi kiwango knachohitajika kisheria na zitendelea na shughuli zake kwa mujibu wa sheria kama kawaida.

“Kutokana na hali hiyo, Wanahisa wa TWB na TPB Bank PLC, wameamua kuunganisha benki hizo ili kuboresha ufanisi na utendaji wa benki hizo, hivyo kutokana na muungano huo kutakuwa na benki moja ambayo itaendelea kuitwa benki ya TPB Bank PLC.

“Benki Kuu imeridhia uuganishaji wa benki hizo kuanzia Agosti 3, mwaka huu ambapo itaendelea kuwa na mtaji wa kutosha kama sheria ya mabenki inayotaka.

“Hivyo wateja, wafanyakazi, mali na madeni yote ya TWB yataunganishwa na TPB, muungano huo utaifanya muungano mpya kuwa imara zaidi na kuwa na mtaji wa kutosha kama inavyotakiwa kisheria, chini ya kifungu cha 17, cha sheria ya mabenki na taasisi za kifedha ya mwaka 2006.

“BoT inawaomba wateja wa TWB kuwa watulivu katika kipindi hiki cha mpito cha uunganishaji wa benki hizi,” amesema Profesa Luoga.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles