23.9 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

AFRIKA KUSINI KUBINAFSISHA ARDHI BILA FIDIA

PRETORIA, AFRIKA KUSINI


RAIS Cyril Ramaphosa amesema chama chake tawala cha ANC, kitahakikisha kinamalizia marekebisho ya katiba ili kuwezesha kuanza mpango wa kuchukua ardhi bila fidia.

Ramaphosa alisema mabadiliko hayo ni muhimu katika maendeleo ya uchumi nchini hapa.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko makubwa juu ya mabadiliko hafifu ya masuala ya ardhi nchini hapa.

Watu weupe ambao ni idadi ndogo ya raia wa Afrika Kusini, wanaaminika kuwa ndio wanashikilia maeneo makubwa ya ardhi na yenye rutuba.

Lakini wakosoaji wa suala hili wanaonya hatua hiyo huenda ikasababisha kile kilichotokea nchi jirani ya Zimbabwe.

Karibu asilimia 10 ya ardhi inayomilikiwa na watu weupe imegawiwa kwa watu weusi tangu kumalizika kwa sera ya ubaguzi wa rangi, suala ambalo ni theluthi tu ya lengo la ANC.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles