23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Barton  asimamishwa  wiki  tatu Rangers

joey-bartonUONGOZI wa  klabu ya  Rangers jana umemsimamisha kwa wiki tatu kiungo wa timu hiyo,  Joey Barton, baada ya kukutwa na hatia ya kupigana na mchezaji mwenzake, Andy Halliday.

Uamuzi huo ulifanyika ikiwa ni siku sita baada ya nyota huyo kurudishwa kwao kutokana na kutuhumiwa kufanya kitendo hicho.

Barton mwenye umri wa miaka 34, alikiri kufanya kitendo hicho katika kikao kilichofanyika jana klabuni hapo.

Kwa mujibu wa Meneja wa klabu hiyo, Mark Warburton, klabu hiyo inahitaji muda na nafasi ya kujadili tatizo hilo.

“Mmoja kati ya Barton au Halliday, anatakiwa kuandaa maelezo kuhusu tukio hilo,” alisema Warburton.

Inafahamika kuwa ugomvi kati ya wachezaji hao  ulitokea  wiki iliyopita wakati timu yao ilipofungwa mabao 5-1 dhidi ya wapinzani wao Celtic.

Baada ya kutokea kitendo hicho, klabu iliwataka  kuondoka na kurejea jana ambapo uongozi wa klabu hiyo ulifanya uamuzi.

Katika utetezi wake, Barton alikiri kukosea na aliomba msamaha kwa kitendo chake cha kumvamia mchezaji mwenzake.

“Miongoni mwa  vitu nilivyofanya havikuwa  sahihi, sikutakiwa kufanya nilichofanya, naomba nisamehewe.

“Kuomba msamaha  haimaanishi kuwa kila siku nitakuwa na makosa na mtu  mwengine atakuwa sahihi, maana yake ni kuongeza uhusiano zaidi kwa wengine,” alisema Barton.

Kosa jingine  alilolifanya nyota huyo  ni kuzungumza katika vyombo vya habari bila kupewa ruhusa na klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles