22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Barnabas kuwatoa wanne wa Bongo Fleva

Barnaba-EliasNA GLORY MLAY

MSANII wa kizazi kipya, Barnaba Elias, yupo mbioni kuwatoa wasanii chipukizi wa kike wawili na wa kiume wawili waliomshirikisha katika viitikio vya nyimbo zao.

Kati ya wasanii hao, ni Aisha Omary ‘Amshapopo’, Mulla na Ice ambapo Mulla na Ice nyimbo zao zimeshakamilika tayari kwa kusambazwa kwenye vituo vya redio, huku Amshapopo na mwenzake wakiendelea kukamilisha nyimbo zao.

Barnaba alisema hakuwahi kufikiria kuwa na wasanii, anachofanya ni kuwasaidia kwa kuwa ana uwezo wa kufanya hivyo na endapo wataweza kusimama wenyewe watakuwa huru kufanya kazi zao.

“Hadi sasa nina wasanii wawili wa kike na wawili wa kiume ambao tayari wameshakamilisha nyimbo zao na wiki hii nyimbo zao zitakuwa hewani kwa ajili ya kupokelewa na mashabiki wao,” alieleza Barnaba.

Hata hivyo, mmoja wa wasanii hao, Asha, alisema baada ya kuhangaika sana kurekodi studio zenye viwango vya chini alilazimika kwenda kwa wasanii wenye majina makubwa katika muziki huo kwa ajili ya ushauri na msaada, lakini walikuwa wakimkwepa na kukataa kumsikiliza hadi alipokwenda kwa Barnaba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles