22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi Mbarouk ateta na Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Nje-EU

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kuzungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Nje za Umoja wa Ulaya (EU), Helena Konig katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ambapo Balozi Mbarouk amemhakikishia, Konig kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika nyanja za biashara na uwekezaji, utunzanji wa mazingira hususan uchumi wa buluu, nishati, miundombinu pamoja na ushirikiano wa kikandaa na kimataifa kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Napenda kukuhakikishia kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika sekta za biashara na uwekezaji, uchumi wa buluu, nishati, miundombinu kwa maslaahi ya pande zote mbili,” alisema Balozi Mbarouk.

Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya kuimarisha maeneo muhimu hususan biashara na uwekezaji kwa kuwa sekta hiyo ni muhimu kwa kukuza uchumi wa pande zote mbili.

Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Huduma za Nje Umoja wa Ulaya, Konig amesema licha ya changamoto ya uviko 19 kuikumba Dunia na vita ya Urusi na Ukraine, Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Afrika, hususan Tanzania kuimarisha na kuendeleza sekta za biashara na uwekezaji.

“EU tunaendelea kushikamana na kuimarisha nguvu zetu kwa pamoja ili kuhakikisha tunaendelea kuwekeza na kukuza biashara kati yetu na Tanzania kwa maslahi ya mataifa yote,” alisema Konig.

Viongozi hao pia wamejadili masuala ya jinsia, digitali, ulinzi na usalama katika ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na kijamii na kisiasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles