BAKWATA:Ugaidi ni kinyume na Uislamu  

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Tanga limesema kuwa    matukio ya mauaji yaliyotokea  Tanga hayahusiani na Uislam kwa vile  vitendo hivyo ni kinyume na  imani ya dini hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari   jana, Sheikh  wa Mkoa wa Tanga, Ali Jumaa Liwuchu aliomba serikali kuhakikisha wahusika wanachukuliwa kama wahalifu wengine.

Sheikh  Liwuchu alikanusha uislam kuhusishwa na matukio hayo akisema dini hiyo haielekezi uovu bali Imani na amani katika jamii.

Sheikh Liwuchu ambaye ni  mwenyekiti wa baraza la amani Mkoa wa Tanga, alilaani matukio hayo na watakaobainika wahesabiwe kama wakosaji wengine na   hakuna dini ya Mungu yenye uhusiano na
uhalifu.

Alisema matukio hayo yanatisha na kutaka wadau wa amani kuisaidia serikali   kuangalia namna bora ya kukabiliana na uhalifu huo ambao unalichafua taifa hili.

Shekh Liwuchu alichukua nafasi hiyo kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki waliopatwa na msiba huo mzito na kuwataka wanaTanga na Tanzania kwa ujumla kuwa wavumilivu wakati serikali ikishughulikia matukio hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here