Muswada kufungia wenye viwanda waja

January MakambaHADIA KHAMIS NA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema inajiandaa kupeleka bungeni muswada wa sheria wa kuwabana wamiliki wa viwanda wanaotiririsha maji machafu.

Akizungumza  katika maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani Dar es Salaam jana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba  alisema muswada huo utapelekwa bungeni Septemba mwaka huu na utaweka adhabu ya kufungia viwanda vitakavyokiuka sheria hiyo.

“Uongozi wa serikali ya awamu ya tano si wa maneno bali ni wa vitendo. Baada ya kupitisha sheria