22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Baharia siyo muhuni bali ni mtaalamu aliyekaa darasani-DMI

*Watanzania wahimizwa kuchangamkia fursa
*Lengo ni kuzalisha Wataalam wa uchumi wa bluu

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Chuo cha Bahari Dar es Salaam(DMI) kimeitaka jamii kuacha dhana ya kufananisha fani ya Ubaharia na uhuni na kuwataka watu kuheshimu fani hiyo.

Adha, chuo hicho kimesema kuwa kwenye nyanja ya bahari bado kuna fursa nyingi hivyo Watanzania wanatakiwa kujitokeza.

Kepteni Hamis Omari Kikuruzo(kulia) akitoa ufafanuzi wa kozi zinazotolewa na Chuo cha Bahari kwa mmoja wa Watanzania waliotembelea Banda la chuo hicho katika Maonyesho ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Julai 20, 2022.

Hayo yamebainishwa na Julai 20, 2022 na Afisa Habari wa chuo cha Bahari(DMI), Edwin Frank wakati akizungumza na Mtanzania Digital katika maonyesho ya Elimu ya Juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) yanayoendelea katika vinjwa vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

“Ukienda mtaani utakuta baharia anajulikana kama ni mtu muhuni muhuni anaeweka kitambaa mfukoni, lakini sisi DMI tupo hapa kwa ajili ya kuondoa hii dhana kwani ubaharia ni taaluma kama zilivyo nyingine.

“Tunapomzungumzia baharia ni mtaalamu ambaye ampeta maarifa anayeweza kuongoza meli lakini pia anaweza kuongoza mitambo, kwani meli inaendeshwa na watu wawili kwa maana ya Injinia anayeangalia usalama wa mitambo na kuna Kepteni ambaye anaangalia mwelekeo au safari inavyoenda na hawa sisi ndiyo tunawazalisha kwenye chuo chetu,” amesema Frank.

Frank amesema kuwa kama fani hiyo ingekuwa ni uhuni basi baharia asingekuwa nakabidhiwa meli iliyojaa makontena yenye thamani kubwa kuongoza hivyo ni vema watu wakaheshimu taaluma hiyo na kuipa hadhi kama zilivyo nyingine.

“Mfano miezi kadhaa nyumba kuna meli kubwa ilitia nanga pale bandari ya Dar es Salaam ikiwa na makontena zaidi ya 4,000, sasa unaweza kufikiria ni kwa kiasi gani unaweza kumpa mtu mhuni vitu vyenye thamani kama hivo, hivyo mtazamo huu unapaswa kuachwa,” amesema Frank.

Akizungumzia taaluma zinazotolewa na chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Frank amesema kuwa kuna kozi za ubaharia na kusisitiza kuwa tasnia hiyo ya bahari bado ina fursa nyingi.

“Katika chuo cha DMI kwanza tunatoa kozi za ubaharia ambazo zina fursa nyingi, lakini hii tasnia ya bahari bado haijajaa ikilinganishwa na nyingine na kama unavyojua sasahivi dunia pamoja na nchi yetu tunazungumzia uchumi wa bluu.

“Kwa hiyo bado kuna uhitaji mkubwa sana, tunahitaji nguvu kazi kubwa sana ambayo itawajibika kuhusiana na nyanja hii ya uchumi wa bluu, bado kuna nafasi kubwa hivyo tunahitaji vijana ambao wanaweza kusomea masuala haya ya ubaharia kwa sababu fursa bado ni nyingi na wataalamu zaidi wanahitajika ili kukidhi mahitaji ya uchumi wa bluu,” amesema Frank na kuongeza kuwa chuo hicho pia kinatoa elimu kuhusu masuala ya mafuta na gesi.

Chuo hicho pia kimehimiza Watanzania kutembelea kwenye banda hilo la DMI katika maonyesho hayo yanatarajia kufikia kilele Julai 23, 2022.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles