23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

‘Kuleta ufanisi bandarini, Serikali isiingie tena mkataba na TICTS’

*Kumesababisha bandari kushindwa kuwa na ufanisi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kutoka na Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania (TICTS) kutowekeza vya kutosha kwenye miundombinu ya Bandari (Equipment,
Logistics corridor, etc.) ufanisi kwenye bandari ya Dar es Salaam umekua mdogo na kulalamikiwa na wadau na viongozi wa juu Serikalini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliikosoa hadharani Bbandari ya Dar es Salaam kwa kukosa ufanisi na kumfuta kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamisi na kumteua, Plasduce Mbossa ambaye ameahidi kuongeza ufanisi wa bandari.

Mwaka 2017 aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli aliiagiza TPA kupitia upya mkataba wa TICTS akisema hauna maslai kwa taifa.

Mwaka uliofuata yaani 2008, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lilipitisha azimio lililoiagiza serikali kubatilisha nyongeza ya mkataba wa TICTS.

Wadau na wafanyabiashara mfano Chama wa Mawakala wa Forodha (TAFFA) wamekuwa
wakilalamika miaka nenda rudi kuhusu TICTS kuwa na ufanisi mdogo na kusababisha
ucheleweshaji wa mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Madhara kwa Nchi:

Ucheleweshaji wa mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam unasababisha sio tu
kero na gharama kwa wafanyabiashara, lakini pia kuongezeka kwa bei za bidhaa nchini na
hivyo kuwaumiza wananchi moja kwa moja.

Hii pia inaenda sambamba na kulikosesha taifa mapato kutokana na wafanyabiashara wa nchi jirani kuamua kuikwepa bandari ya Dar es Salaam na kukimbilia bandari za Kenya, Afrika Kusini na Namibia zenye ufanisi zaidi. Wakati bandari ya Dar es Salaam yenye kila faida kuanzia Kijiografia.

Takwimu za mwaka 2019 zinaonyesha kwamba Bandari ya Dar es Salaam inapata kontena 600,000 kwa mwaka, bandari ya Mombasa yenyewe ilipata kontena million 1.4 huku lengo likiwa ni kufika milioni 2 mwaka 2022 na kuwa bandari kitovu kwenye Pwani ya Afrika Mashariki.

Kudumaza ukuaji wa bandari ya Dar es Salaam ambayo ienelenga kuongeza mzigo wa kontena asilimia 37 kwa mwaka. TICTS imeshindwa kabisa kwenye hili – kati ya 2020 na 2021 TICTS haikuweza kufikia ongezeko la hata asimilia moja (ongezeko lilikua 0.8%).

Viashiria vya ufisadi na ushawishi wa kiasiasa

Mwaka 2005 wakati TICTS ikiwa nusu tu ya mkataba wake, mkataba huo uliongezwa kwa
miaka 15 licha ya malalamiko ya dhidi ya utendaji mbovu katika upokuaji na upakiaji wa
mizigo na upotevu wa mapato ya serikali.

Pamoja na bunge kupitisha azimio mwaka 2008 lililoiagiza serikali kubatilisha nyongeza ya
mkataba wa TICTS, serikali haikuwahi kutekeleza azimio hilo.

Repoti zaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) zimekuwa zikibainisha mapungufu kwenye mkataba wa TICTS na kuishauri serikali kupitia upya mkataba huo kwa lengo la kuhakikisha kuwa maslai ya umma yanalindwa.

Baadhi ya Wanahisa wa ndani wa TICTS wamekuwa wakinyooshewa kidole kwa kashfa za
ufisadi siku za nyuma.

Na sasa mkataba unavyokaribia kuisha na Rais ameshaonyesha nia ya kusafisha na
kuongeza ufanisi bandarini, TICTS inafanya juhudi waongezewe mkataba mwingine wa
miaka mitano licha ya kushindwa kuleta ufanisi kwa zaidi ya miaka 20.

Jitihada hizi zisizo na maslahi kwa taifa zimekuwa zikitajwa kufanyika chini kwa chini ikiwamo kushawishi baadhi ya vyombo vya habari ili kujisafisha.

Serikali isiingie tena mkataba na TICTS:

Tanzania inategemea sana bandari ya Dar es Salaam ambapo takriban asilimia 90 ya biashara zinapita hapo. pia kwasasa bandari hiyo ndio kitovu na inayopendelewa
zaidi na nchi jirani (DRC, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na nyingine) kwa sababu ina nafasi nzuri ya kijiographia.

Hivyo, kuendelea kukumbatia uzembe wa TICTS ni kuhujumu uchumi wa taifa kwa kupoteza mapoto, kusabisha harasa na bei za juu kwa wanachi na kupoteza
nafasi ya kiushindani ya bandari ya Dar es Salaam.

Kwa miaka 20, TICTS imeshindwa kutimiza ndoto ya Watanzania ya kuwa na bandari yenye
ufanisi na ushindani.

Ni muda sasa wa kuwapa nafasi kampuni nyingine zenye ufanisi mzuri (Competitive track Record in Port Operations) watakaoleta ufanisi na wenye network kubwa
duniani kuongeza idadi ya mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa manufaa ya bandari na taifa kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles