23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

TMA yawataka Watanzania kuzingatia tahadhari zinazotolewa

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA) imewataka Watanzania kuzingatia tahadhari zinazotolewa na Mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kufata ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya katika kipindi hiki cha baridi kali ili kuepuka madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza.

Akitoa ushauri huo jana jijini Dar es Salaam Mtaalamu na Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka Kitengo Kikuu cha Utabiti TMA, Rose Senyagwa wakati akizungumzia mvua zinazondelea nchini hususan katika maeneo ya Ukanda wa Pwani.

Senyagwa amesema kuwa mvua zinazoendelea katika ukanda huo pamoja na baadhi ya maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki zimesababishwa na upepo wenye unyevuunyevu unaovuma kutoka bahari ya hindi kuelekea katika maeneo ya nchi yetu na hivyo kusukuma unyeunyevu huo.

‘Mvua zinazoendelea katika maeneo ya ukanda wa Pwani nikimaanisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Kaskazini mwa Morogoro, Lindi, Mtwara, Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na baadhi ya Nyanda za Juu, Kaskazini Mashariki mwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara zimesababishwa na upepo wenye unyevuunyevu unaovuma kutoka bahari ya hindi,” amesema Senyagwa.

Alisema mvua hizo zilianza mwezi Juni katika kipindi cha Kipupwe na zimekuwa zikijitokeza kwa mvua za kawaida hivyo wameziita mvua za nje ya msimu na wanatarajia zitaendelea kuwepo katika kipindi cha Mwezi July mpaka Agosti mwaka huu.

Amesema kutokana na utabiri wa msimu wa kipupwe ambao ulitolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa mwishoni mwa mwezi Mei, maeneo mengi ya nchi yalitarajiwa kuwa na vipindi vya baridi na upepo mkali.

“Katika maeneo ya ukanda wa Pwani na Maziwa Makuu kujitokeza upepo unaofikia Kilomita 40 au kuzidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika mita mbili yanatarajiwa kuendelea kujitokeza,” amesema Senyagwa.

Ameongeza kuwa ni vyema katika kipindi hichi cha baridi na upepo mkali wananchi wakazingatia tahadhari zinazotolewa kwa kujikinga ili kujihadhari na madhara ya kiafya.

Hata hivyo, TMA imewashauri wananchi wanaofanbya shughuli zao kuendelea kuchukua tahadhari kipindi cha upepo mkali ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles