25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Babawatoto yatoa elimu ya corona kwa watoto

Mwandishi Wetu -Dar Es Salaam                             

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Babawatoto (Babawatoto Organization), limetoa ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Elimu hiyo imetolewa kwa watoto hao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto anayeishi na Kufanya kazi Mtaani ambayo huadhimishwa Aprili 12 kila mwaka.

Mkurugenzi wa shirika hilo, Mgunga Mwamnyenyelwa amesema lengo la siku ni kujenga ushawishi kwa wanajamii na serikali kuwekea mkazo zaidi suala la haki na ustawi wa watoto wakiwamo wanaoishi na kufanya kazi mtaani.

“Maadhimisho ya mwaka huu yameanza Aprili 8, lakini kutokana na changamoto ya ugonjwa ya corona kama shirika tumelezimika kuwakumbuka watoto wa mtaani kuwapa elimu.

“Lakini yale ya msingi kwa Jamii tumekuwa tukitumia vyombo vya habari kuwafikishia ujumbe wanajamii badala ya kuwakusanya watoto pamoja kama zamani, hii ni njia pia ya kuwalinda na ugonjwa huo hatari,” alisema Mgunga.

Pamoja na mambo mengine alisema shirika la Babawatoto linatekeleza mradi wa ‘Kizazi Kipya’ ambao unalenga kutetea haki za watoto na vijana wanaoishi na kufanya kazi mtaani  ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za Kibinadamu kama afya ikiwamo kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) na kuhudumia wenye VVU na Ukimwi, kuwapa chakula na elimu ya msingi na ufundi ili hatimaye wajitoe kwenye maisha ya mtaani.

Alisema mradi huo ambao uko chini ya Pact Tanzania na  Railway Children Africa (RCA)  kwa ufadhili wa mashirika ya misaada ya USAID la Marekani na  UKAID la Uingereza tangu mwaka 2017 umehudumia jumla ya watoto 1,914 wakiwamo wasichana 352 na wavulana 1,562 ambao wengine waliunganishwa na wanafamilia.

“Ujumbe wa mwaka huu unaitaka jamii kutambua kwamba watoto wote wanastahili kujisikia kuwa salama hivyo jamii yote iwajibike, watoto wana haki ya kulindwa dhidi ya  vurugu na manyanyaso pasipo  kujali  wanatoka katika maisha ya aina gani, jamii  kuchukua hatua zaidi  katika kuwezesha ulinzi wa mtoto anayeishi mtaani kwani maranyingi mtoto huyu husahaulika,” alisema Mwamnyenyelwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles