30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kutoa mwongozo waliosimamishwa kazi

Ramadhan Hassan -Dodoma

SERIKALI imesema itatoa maelekezo nini kifanyike ili kila mmoja aweze kufahamu msimamo wa Serilali kuhusiana na wafanyakazi wa sekta binafsi  ambao wamesimamishwa kazi  kutokana na  ugonjwa wa corona.

Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya wafanyakazi hususani katika Mahoteli kulalamika kwamba wamesimamishwa kazi huku waajiri wakishindwa kuwalipa mishahara   hali ambayo imesababisha maisha kuwa magumu kwao.

Hayo yalielezwa jana Jijini hapa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana, Anthony Mavunde   wakati alipokuwa akifanya  mahojiano na kituo kimoja cha luninga ya mtandaoni.

Mavunde alikuwa akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji wa kipindi, kwamba baadhi ya makampuni binafsi kuwaondoa wafanyakazi pasipo kuzingatia utaratibu kwa sababu ya ugonjwa wa corona.

Akijibu, Mavunde alisema katika hilo msimamo wa Serikali utabainishwa hivi karibuni  ili kila mwajiri aweze kuzingatia miongozo kwani Ofisi ya Waziri Mkuu inaendesha masuala ya wafanyakazi kwa utatu akimaanisha wafanyakazi,waajiri na Serikali.

“Na ninavyozungumza na wewe kikao cha pamoja kimekaa wiki iliyopita  na tunasubiri maazimio na tutatoa maelekezo nini kifanyike  lakini tulikaa kwa pamoja na tumewashirikisha wote kwa pamoja ili kila mmoja aweze kufahamu msimamo wa Serikali ni upi,”alisema Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini(CCM).

Alisema mkakati wa Serikali ni kuendelea kuwasaidia vijana kwa kuhakikisha wanatimiza ndoto zao  katika mambo mbalimbali.

“Lazima kutafuta suluhisho la kila mmoja kwa hiyo hatua ya kwanza ni kutambua kwanza makundi hatua ya pili tumeendelea kuwasisitiza kukaa kwenye makundi ili kusaidika na tumewatoa kwenye vikundi na tumeenda kwenye makampuni.

“Mkakati wa Serikali ni kutengeneza makundi ya kufanya shughuli za kiuchumi na hatua ya tatu ni  lazima tuwatengenezee ‘Programu’ za kukuza uchumi,kijana wa Tanzania akijengewa mazingira ya kuwa na ujuzi utamsaidia,” alisema.

Naibu Waziri huyo wa Kazi,Ajira na Vijana alisema kwa sasa Serikali ina programu ya  urasimishaji ujuzi kwa wenye ujuzi ambao hawakupitia mfumo rasmi wa mafunzo ya ufundi ambao umewasaidia vijana wengi kuweza kutambulika.

“Serikali inapeleka mafundi wa Veta mtaani kuwatafuta hawa wenye ujuzi ambao wapo mtaani kwani huyu  akienda kuomba kazi anaulizwa umesoma wapi na tumesaidia kuwarasimisha na wamepata  vyeti,”alisema Mavunde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles