30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dada wa Balali afutiwa kesi, afunguliwa mashtaka mapya

KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubali kumfutia kesi ya uhujumu uchumi dada wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, marehemu Daudi Balali, Elizabeth Balali (54) baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuomba kufanya hivyo.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa leo Jumanne Arili 14, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kuwasilisha maombi ya kuondoa mashtaka baada DPP kuona haoni haja ya kuendelea nalo.

Hakimu Isaya alikubali maombi hayo na kuamuru kesi iondolewe na mshtakiwa aachiwe huru katika shauri hilo.

Mshtakiwa huyo alikuwa anadaiwa kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 jijini Dar es Salaam alijipatia kiasi cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk. Roderick Kisenge kwa ulaghai.

Inadaiwa alijipatia fedha hizo baada ya kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambazo halijapimwa lililopo eneo la Boko Dovya Kinondoni wakati akijua eneo hilo si lake.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha, inadaiwa kuwa katika kipindi hicho mshtakiwa huyo alipokea kiasi hicho cha Sh milioni 25 kutoka kwa Dk. Kisenge kupitia akaunti yake iliyopo katika Benki ya CRDB wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kufutiwa mashtaka hayo, mshtakiwa huyo alifunguliwa mashtaka mapya ambapo alirudishwa mahabusu akisubiri kusomewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles