28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Babati wapokea fedha za EP4R

Na JULIETH PETER-BABATI

HALMASHAURI ya Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara, imepokea Sh milioni 97 kutoka katika Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) awamu ya saba, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule mbili za msingi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Hamisi Malinga, aliyasema hayo hivi karibuni katika kikao cha Baraza la Madiwani.

Kwa mujibu wa Malinga, fedha hizo zilipokelewa Juni mwaka jana na kuelekezwa katika shule za msingi za Quash na Riroda kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na matundu 6 ya vyoo.

“Shule hizo za msingi zimepangiwa jumla ya shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, shilingi milioni 6.6 kwa ajili ya ujenzi wa matundu sita ya vyoo na shilingi milioni mbili kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji.

“Pamoja na hayo, ni kwamba hizo shilingi milioni 40 kwa ujenzi wa madarasa mawili kwa kutumia ‘force account’, kuna uwezekano wa kuzitumia kujenga madarasa zaidi ya mawili.

“Kwa hiyo, nawaomba madiwani wajikite katika kutumia force account itakayowawezesha wananchi kushiriki kikamilifu kutekeleza miradi hiyo na kupunguza upungufu wa madarasa.

“Kwa ujumla, uboreshaji wa miundombinu ya shule utasaidia wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao kwani matokeo ya upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili, kidato cha nne na upimaji wa darasa la nne, umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kuboreshwa kwa miundombinu hiyo,” alisema Malinga.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu, aliwataka viongozi wote kuanzia ngazi ya kata, vijiji na wilaya, kuifanya ajenda ya utoaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi, kuwa ajenda ya kudumu na izungumziwe katika vikao mbalimbali na mikutano ya kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles