24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama nchini zatakiwa kutenda haki

Na AMINA OMARI-TANGA

MAHAKAMA nchini imeshauriwa kuwa sehemu ya kimbilio la wanyonge katika upatikanaji wa haki kwa wakati, ili jamii iendelee kuwa na imani ya uwepo wa chombo hicho.

Ushauri huo umetolewa wiki iliyopita na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, wakati wa kilele cha wiki ya sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga, iliyopo jijini Tanga.

Alisema kama mahakama itatimiza wajibu wake, migogoro mingi ambayo ingeweza kupatiwa haki kwa wakati, itaweza kumalizwa na kujenga jamii imara na yenye amani.

“Tunajua kwamba, migogoro inaweza kutatuliwa kwa njia mbili za usuluhishi au kwa njia ya mahakama. Hivyo basi, ni wajibu wa idara ya mahakama kuhakikisha inatenda haki ili iwe kimbilio la wanyonge wengi ambao wamekuwa ni waathirika kwa kunyimwa haki zao,” alisema Mwilapwa.

Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga, Amir Mruma, alisema mwaka jana peke yake, jumla ya mashauri 2,491 yalifunguliwa mkoani Tanga.

Alisema kwamba, mashauri hayo ambayo yalifunguliwa katika ngazi mbalimbali mkoani hapa, yalikamilika kwa asilimia 97 na kwamba asilimia tatu zilizobaki zitakamilika wakati wowote kuanzia sasa.

“Hata hivyo, mwaka huu tumejipanga kuhakikisha tunatoa kipaumbele kwa mashauri ambayo yana mvuto kwa jamii ili kujenga imani kwa jamii na kuwafanya wananchi waone umuhimu wa chombo hicho cha mahakama.

Naye Msemaji wa Ofisi ya Mashtaka, Mkoa wa Tanga, Peter Maugo, alisema changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kwa sasa ni kuahirishwa kwa kesi bila sababu za msingi, hali inayochangia

ucheleweshaji wa baadhi ya mashauri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles