Azam yaapa kutetea ubingwa Kagame

0
943

Na Jessca Nangawe

BAADA ya kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali michuano ya Kombe
la Kagame inayoendelea nchini Rwanda, benchi la ufundi la Azam FC
limetamba kwamba watahakikisha wanatetea ubingwa wao.

Akizungumza na Dimba, kocha Mkuu wa kikosi hicho Etienne
Ndayiragije, alisema vijana wake wapo tayari kwa mapambano, lengo likiwa ni kufanya kweli na kurudi Dar es Salaam na ubingwa.

“Michuano hii ni migumu kwani timu zote shiriki zinaonekana
kujiandaa vizuri.

“Tunamshukuru Mungu kwamba tumefika hatua ya
robo fainali na kilichopo ni kupigana kiume tutetee ubingwa wetu,” alisema.

Kikosi hicho cha Azam FC kimewasili jijini Kigali, Rwanda jana Jumamosi saa 7 mchana, tayari kwa mechiya robo fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Kagame wiki ijayo.

Azam FC imetokea mjiniHuye, Rwanda ilipokuwa ikicheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kabla ya juzi Ijumaa kufuzu kwa
robo fainali ikiwa na KCCA ya Uganda katika hatua ya makundi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here