Azam FC waanza tambo mapema kwa Yanga

0
791

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

BAADA ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli FC, Kocha msaidizi wa Azam, Idd Nassor ‘Cheche’, amesema wamepata morali ya kuendeleza vichapo katika mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga, unaotarajiwa kuchezwa Jumapili Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Azam juzi walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Cheche alisema amefurahi kuona wachezaji wake wamefuata kile walichowafundisha hivyo wataendelea kupambana katika mechi zilizopo mbele yao.

“Mchezo ulikuwa mgumu lakini utulivu ndio umefanya tuweze kupata ushindi, hivyo kwa sasa tunaenda kujiandaa kwa ajili ya mechi inayotukabili mbele yetu dhidi ya Yanga ili tuweze kuvuna pointi tatu muhimu,” alisema.

Alisema mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa ukizingatia wapinzani wao wametoka kufungwa, hivyo lazima wawe makini zaidi kuhakikisha wanaendeleza ushindi.

Cheche alisema watatumia uzembe wa wapinzani wao ili wapate mwanya wa kufunga kwani kila mmoja atakuwa akihitaji ushindi.

Alisema kwa sasa wanakwenda kuyafanyia kazi baadhi ya kasoro zilizojitokeza katika mchezo wao uliopita ili zisijirudie Jumapili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here