MREMBO anayefanya vizuri katika video za Bongo Fleva, Asha Salum ‘Kidoa’ amesema tasnia ya urembo nchini
inachafuliwa na wasichana wachache wasioitakia mema tasnia hiyo.
Akibonga na Swaggaz, Kidoa alisema kuwa mara kwa mara warembo wanao onekana kwenye video za muziki wamekuwa hawapati heshima inayostahili kutokana warembo hao kutafuta umaarufu kinguvu.
“Ni bora ukatafuta sehemu nyingine ya kutafuta umaarufu usio na faida kuliko kuingia kama Video Queen kisha unaanza kuidharirisha tasnia yetu, tumekuwa hatupati heshima kutokana na wachache wanaotuchafua,”
alisema Kidoa
Mrembo huyu alianza kuonekana kwenye video ya msanii Ney Wa Mitego kwenye wimbo wa Akadumba kisha akapata nafasi y kupendezesha video ya Profesa Jay katika wimbo wa mili Gado.