Kidoa atoa ya moyoni

0
826

Miriam-Jack-Artwork1-750x750MSANII wa nyimbo za Injili nchini, Miriam Jackson amewataka wasanii wa muziki huo wajiongeze kwa kufanya kazi zenye ubora licha ya kuwa wanafanya huduma ya Mungu.

Akipiga stori na Swaggaz, Miriam Jackson alisema kuwa kumekuwa na dhana kwamba muziki wa Injili ni wa kujitolea hivyo ubora wa kazi si jambo la kulizingatia sana kitu ambacho kimekuwa kikiipotosha tasnia hiyo.

“Hii ni huduma ya Mungu lakini haimaanishi ifanyike kwenye mazingira ya kizamani, huu ni wakati wa wasanii wenzangu kujiongeza kwa kufanya kazi bora wasiongope kutumia gharama ili kulitangaza neon la Mungu,” alisema Mirium.

Alitoa mfano kuwa yeye hakujali ghalama ndiyo maana alisafiri mpaka nchini Kenya kwenda kufanya video ya wimbo wake unaoitwa Ni Bwana aliomshirikisha Goodluck Gozbert.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here