23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu Shoo atoa ujumbe wa Uchaguzi Mkuu

Na Safina Sarwatt- Kilimanjaro

MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Askofu Dk. Fredrick Shoo, amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani na upendo katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu. 

Dk  Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kasikazini, aliyasema hayo jana wakati wa akifungua mkutano mkuu wa 36 wa dayosisi hiyo.

“Mtu muovu kupita wote ni yule anayeruhusu watu waovu kutawala,”alisema Shoo. 

Alisema wakati Serikali inaelekea katika Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na udiwani ni nafasi ya kipekee na kikatiba anayopewa raia kuchagua kiongozi bora ama kuchaguliwa kuwa kiogozi. 

“Wakristo ni wenyeji wa duniani na mbiguni wakati ule ule, kwahiyo tuwapo hapa duniani inatupasa kukiriki kwa uadilifu yale yampasayo raia wa dunia hii. 

“Ninawahimiza wakristo na watu wote kukishiriki kwa haki, usawa, uwazi, amani na utulivu katika mchakato wa kuwapata viongozi, “alisema Dk. Shoo. 

Alisema wakati wa kampeni za uchaguzi wananchi wawasikilize wagombea ili kupata ufahamu kama wanasifa sahihi za kuwa viongozi bora na kufanya uchaguzi sahihi Oktoba 28.

“Ni kweli kuwa sisi viongozi wenu hatupaswi kuwa washabiki wa chama fulani, lakini ni wajibu wetu kuwasaidia watu kupata ujuzi wa kweli kuhusu anayefaa kuwa kiongozi, tufanye hivyo tukishirikiana na Serikali na wengine wote wenye mapenzi mema, tuwachague wanaofaa na siyo chama, “alisema. 

Askofu shoo pia aliwataka wanasiasa, viongozi wa dini zote na Watanzania kwa ujumla kudumisha haki, amani na utulivu, kwani  hizi tunu za pekee katika maisha na taifa hili. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira alisema mkutano huo umeandaliwa katika kipindi maalumu na kulopongeza kanisa kuendelea kushirikiana na Serikali hasa  wakati taifa ikielekea katika Uchaguzi Mkuu. 

Alisema tayari vyama vyote vimeshaanza mchakato wa kuwapitisha wagombea wao hivyo kutaka wananchi kuendelea kushikamana ili kukamilisha Uchaguzi Mkuu kwa amani na upendo.

Alisema pamoja na mambo mengine wataendelee kuugana hata katika kazi za umma na kijamii, kwani wote  wanajenga moja.

Kwa upande wake Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini, Martine Shao, aliwataka Watanzania kuendelea kuwaenzi wastaafu na kufauta yale maelekezo waliokuwa wakiyaelekeza. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles