24.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

ARSENE WENGER MWISHO WA ENZI MIAKA  22  YA  JASHO, MACHOZI NA DAMU

 

LONDON, ENGLAND


WAKATI ni ukuta ukishindana nao utaumia ni kauli ambayo Mfaransa Arsene Wenger ameutumia baada ya kuhisi kuwa muda sio rafiki wake tena katika majukum yake ya kukiongoza kikosi cha Arsenal.

Baada ya kudumu kwa miaka 22 akiwa na kikosi cha Arsenal,  hatimaye wakati umefika kwa kocha Wenger, kukubali yaishe mwishoni mwa msimu.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 68, aliamua kupigana vita na nafsi yake ambayo iliamini kuwa Arsenal ndio nyumbani kwake.

Hii huenda ikawa ni furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao walianza kupotea kwa kasi viwanjani baada ya kuchoka kubeba mabango ya kumuondoa kinguvu kocha huyo

Wenger alianza kuwanoa ‘Washika Mitutu’  wa London mwaka 1996 akitokea klabu ya Nagoya Grampus Eight ya Japan.

Alitua katika kikosi hicho akiwa ni kocha wa 26 kuinoa timu tangu mwaka 1898 huku kocha wa kwanza kuinoa timu hiyo alikuwa, Thomas Mitchell raia wa Scotland.

Katika kipindi chote alichodumu katika timu hiyo , Wenger amefanikiwa kunyakua mataji matatu ya Ligi Kuu kuanzia msimu wa 1997/98, 2001/02, 2003/04, wakati huo Kombe la FA wakichukua mara saba tangu mwaka 1997/98, 2001/02, 2002/03, 2004/05, 2013/14, 2014/15, 2016/17, pamoja na kombe la Ligi mara tatu.

Miongoni mwa watu wa kwanza kupata taarifa za kocha huyo alikuwa nahodha wa kikosi hicho,  Per Mertesacker, ambaye amekuwa mtu muhimu kwa kocha huyo.

“Nina furaha kwa historia ya kukumbukwa ambayo nitakuwa ninaiacha katika klabu hiyo kutokana na kuwa hapa kwa miaka mingi, nilitumia uwezo wangu wote kuhakikisha naweza kuisimamia klabu hiyo.

“Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru viongozi, wachezaji, pamoja na mashabiki kwa kuifanya klabu hii kuwa muhimu hasa katika kuipigania ili iweze kuwa katika nafasi ya juu.

“Kwa wale wapenzi wa klabu ya Arsenal, nawaambia wawe makini na thamani ya klabu, nitaendelea kuwa mpenzi wa Arsenal na nitaendelea kutoa sapoti hadi mwisho wa maisha yangu,” alisema Wenger.

Makocha wanaopewa nafasi ya kumrithi

Baada ya kocha huyo kutangaza azma yake ya kuachana na timu hiyo tayari baadhi ya makocha wameanza kutupiwa macho huenda wakarithi kiti cha Mfaransa huyo.

Miongoni mwa makocha wanaopewa nafasi kubwa ni pamoja na kocha wa zamani wa Main o4 na Borussia Dortmund, Thomas Tuchel, ambaye hivi sasa hana timu mwingine ni kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ujerumani, Joachim Low.

Wengine ni  kocha wa zamani wa Celtic ambaye pia aliwahi kupita katika klabu ya  Liverpool, Brendan Rodgers, huku vijana waliowahi kupita katika mikono yake Patrick Vieira pamoja na Thiery Henry pia wakiwa katika orodha hiyo.

Nyota wake wamlilia

Baadhi ya wachezaji wameshindwa kuzuia hisia zao miongoni mwao ni kiungo wa klabu hiyo Jack Wilshere, ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa hawezi kumsahau kocha huyo kwa kitendo cha kumuamini tangu akiwa na miaka 16 hadi hivi sasa.

Mwingine ni mlinzi wa kulia wa zamani wa klabu hiyo Bakary Sagna, ambaye aliandika kuwa kocha huyo ni mtu muhimu zaidi kwani ndiye aliyempa maisha yeye pamoja na familia yake kwa kumpa nafasi katika kikosi chake.

Ferguson alonga

Licha ya kukwaruzana mara kadhaa alipokuwa akikinoa kikosi cha Man United, lakini kocha huyo amemmwagia sifa kocha huyo kwa mafanikio aliyoyapata akiwa na kikosi hicho kwa miaka 22 aliyodumu kutoka Highbury hadi Emirates.

Ifuatayo ni michezo ambayo imesalia kwa kocha huyo kusimama katika benchi la timu hiyo kabla ya kutimka na kuanza maisha sehemu nyingine.

Atakuwa na kibarua mbele ya Atletico Madrid , Aprili 26 katika michuano ya Europa, Aprili 29 dhidi ya Manchester United, Mei 3 wakipambana na Atletico Madrid.

Wakati michezo mingine itakuwa dhidi ya Burnley Mei 6, Mei 9 wakicheza dhidi ya Leicester City na atakamilisha kibarua chake na wabishi Huddersfield, Mei 13.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles