29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Arsene Wenger atakiwa kuondoka Arsenal

WENGERLONDON, ENGLAND

BAADA ya Arsenal kupokea kichapo kwenye Uwanja wa nyumbani wa Emirates, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Olympiakos, mashabiki wa klabu hiyo wamemtaka kocha wao, Arsene Wenger kuachia ngazi.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa mwanzoni mwa wiki hii, Arsenal ilikubali kichapo cha mabao 3-2 na kuifanya klabu hiyo kushika nafasi ya mwisho katika kundi F ikiwa haina hata pointi na wakitarajia kukutana na Bayern Munich katika mchezo wao wa tatu.

Mashabiki wa Arsenal hawana uhakika wa kusonga mbele katika michuano hiyo, japokuwa kocha huyo anaamini atakuja kufanya vizuri hasa katika mchezo dhidi ya Bayern ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja katika Ligi Kuu nchini Ujerumani na Ligi hiyo ya Mabingwa.

Kupitia mtandao wa klabu hiyo, mashabiki zaidi ya 400 wametuma ujumbe wao wa kumtaka kocha huyo kuondoka, huku wakidai kuwa huu ni muda wa mabadiliko.

“Huu ni muda wa mabadiliko, fanya mambo sahihi halafu uondoke kocha Wenger, tumekuwa na kipindi kigumu kwa sasa kuanzia kwenye michuano ya Ligi kuu na Ligi ya Mabingwa, lakini tunaona hakuna la zaidi,” walisema mashabiki hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles