28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Jose Mourinho ashambuliwa na mashabiki, kisa Terry

jose-mourinho_epa_2587091kLONDON, ENGLAND

MASHABIKI wa klabu ya Chelsea wamemtupia lawama kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho, baada ya kumuweka benchi beki wake, John Terry katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Porto.

 

Mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Dragao nchini Ureno, Chelsea ilikubali kichapo cha mabao 2-1, huku beki wake akiachwa benchi na kocha huyo.

 

Kitendo hicho kiliwafanya mashabiki watume ujumbe mbalimbali katika klabu hiyo wa kudai kwamba wanamtaka beki huyo kupewa nafasi ya kuanza kama ilivyo mwanzo.

Hata hivyo, wakati mchezo huo unaendelea baadhi ya mashabiki walionekana wakiwa na mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yanasomeka ‘tunamtaka nahodha wetu katika kikosi’.

Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand, baada ya kumalizika kwa mchezo huo aliongea kupitia kitua cha utangazaji nchini England na kusema kuwa kikosi hicho kilikosa mchezaji ambaye ni kiongozi kama Terry na kilikosa umoja na ushirikiano.

Terry amekuwa na mchango mkubwa katika klabu hiyo kwa miaka mingi, lakini kwa sasa kocha huyo ameanza kumuacha benchi katika baadhi ya michezo, huku Chelsea ikiwa inapoteza michezo hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles