24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

ANNA MGWIRA ATEMBELEA WANAFUNZI WALIOANGUKIWA NA PAA LA SHULE

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira ametembelea hospitali ya wilaya ya Hai na kuwajulia hali wanafunzi  watatu wa shule  msingi Kibohehe waliojeruhiwa  wakati wa tukio  la kuezuliwa paa la shule hiyo kutokana na  mvua iliyoambatana na upepo .

Wanafunzi   hao waliojeruhiwa sehemu mbalimbali  za mwili ni Mary Herieli Swai (11), Aloyce Abeli (13) na Lukana Abuu (9) wote wanasoma darasa la  tatu katika shule hiyo.

Mghwira aliwatembelea watoto hao  baada ya ukaguzi wa shule hiyo ambapo alisikitishwa na ujenzi usiokidhi vigezo uliosababisha hasara pamoja na kumpoteza mwanafunzi wa darasa la  sita Derich Albarth.

Mkuu huyo wa Mkoa aliwapa pole wanafunzi  wote watatu pamoja na Wazazi wao  waliokuwa  wakiwauguza na kuwataka kuwa wavumilivu wakati serikali ikiendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo halisi ili wahusika wachukiliwe hatua.

Wanafunzi hao wanaendelea na matibabu na hali zao  zinaendelea kuimarika

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles