23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

RACHEL ATAMANI KUITWA MAMA

NA JESSCA NANGAWE


MSANII wa muziki nchini, Rachel Haule, amesema moja ya mikakati yake mwaka huu ni kuona anaitwa mama kama ilivyo kwa rafiki yake wa karibu Linah Sanga.

Rachel amesema maamuzi ya kupata mtoto yametokana na ukaribu wake na Linah ambaye naye aliingia kwenye orodha ya wasanii wenye watoto, baada ya kujifungua mtoto wa kike aliyempa jina la Tracey.

Akizungumza na MTANZANIA, Rachel alisema yupo kwenye mikakati hiyo kwa mwaka huu na anaamini utakuwa na mafanikio kwake kwa kuwa moja ya mambo anayotamani kuyaona ni kupata mtoto.

“Kuwa mama ni bahati sana, moja ya ndoto zangu mwaka huu ni kupata mtoto ili nije kuitwa mama kama ilivyo kwa rafiki yangu Linah na wengine, amenipa motisha kubwa sana, hivyo nipo tayari kwa hilo na naamini Mungu atanisimamia,” alisema Rachel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles