22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Amuua mpenzi wake baada kumfuma akinywa ARV kwa kificho

KAMPALA, UGANDA

MWANAMKE mmoja katika wilaya ya Hoima mashariki mwa Uganda anashikiliwa kwa madai ya kumuua mpenzi wake baada ya kumfuma akimeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV)

Wakielezea tukio hilo, Polisi walisema kuwa, Emmanuel Tumusiime mwenye umri wa miaka 35 alishambuliwa hadi kuuawa katika makazi yake akiwa mji wa Kigorobya saa 12 jioni siku ya Jumatano wiki hii.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la  nchini Uganda, msemaji wa polisi wa mji huo, Julius Hakiza amesema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa Tumusiime alipigwa kichwani na shoka.

”Alipogundua kwamba mpenzi wake amefariki, mshukiwa alifunga nyumba na kupanda bodaboda hadi kwenye kituo kikuu cha polisi cha Hoima na kuripoti kesi ya mauaji,” alieleza Hakiza.

Katika kituo hicho cha polisi, mwanamke huyo alikiri kumuua mpenzi wake.

Mwanamke huyo anadai kuwa alijisikia uchungu sana baada ya kuhisi kuwa kuna uwezekano ameambukizwa virusi vya Ukimwi.

Alikamatwa na kushikiliwa kwenye kituo kikubwa cha Hoima akishutumiwa kwa kujihusisha na mauaji.

“Wapelelezi walikimbilia eneo la tukio na kulifunga kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” alieleza Hakiza.

”Tunatoa wito kwa waathirika wa virusi vya Ukimwi mara zote kuwapa taarifa wenza wao na kuhudhuria vituo vya ushauri nasaha na kufahamu kwamba kwa kuwa mwathirika, haimaanishi ni mwisho wa maisha,” alishauri Hakiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles