28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Pep Guardiola kuondoka Man City

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Manchester City, PepĀ Guardiola, anaweza kuondoka ndani ya kikosi mwishoni mwa msimu huu na nafasi yake inatajwa kuwa inaweza kuchukuliwa na aliyekuwa kocha wa timu ya Tottenham, Mauricio Pochettino.

Msimu uliopita Guardiola aliongeza mkataba mpya ambao utamfanya awe hapo hadi 2021, lakini ndani ya mkataba huo kuna kipengele ambacho kinamruhusu kocha huyo kuondoka mwisho wa msimu kama ataamua na kufikia makubaliano na uongozi wa timu hiyo.

Hata hivyo uongozi wa timu hiyo ya Manchester City unaamini bado kocha huyo ataendelea kuwa hapo bila ya kujali mwenendo mbaya msimu huu katika mbio za kutetea ubingwa.

Hadi sasa Manchester City wapo nyuma kwa pointi 14 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu England, Liverpool, hivyo Man City wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 32, wakati huo Liverpool wakiwa na pointi 46, nafasi ya pili ni Leicester City wenye pointi 38 baada ya kucheza michezo 16.

Inasemekana kuwa sababu kubwa ambayo itamfanya kocha huyo kuondoka ni kutokana na kupoteza mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya wapinzani wao Manchester United mwishoni mwa wiki iliopita kwenye uwanja wa nyumbani Etihad.

Kichapo hicho kimeifanya Manchester City kuwa katika wakati mgumu wa kuchukua ubingwa huo mara tatu mfululizo.

Guardiola amekuwa mmoja kati ya makocha wenye uwezo mkubwa wa kufundisha soka, alianza maisha yake ya kufundisha katika klabu ya Barcelona ambapo alifanikiwa kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu Hispania pamoja na mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kipindi cha miaka minne aliyokaa kabla ya kwenda kujiunga na timu ya Bayern Munich.

Akiwa ndani ya Bayern kwa kipindi cha miaka mitatu alifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu nchini humo kila msimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles