BAADA ya kutangaza kwamba hana mpango tena wa kutoka kimapenzi na wasanii wa muziki wa hip hop, mwanamitindo, Amber Rose, ameamua kutoka na nyota wa mchezo wa kikapu.
Mwezi uliopita mrembo huyo alisema amechoka kutoka na wasanii wa muziki na kilichobaki ni kutafuta mchumba ambaye ni mwana michezo na sasa amefanikiwa kumnasa kijana mwenye umri wa miaka 25, wakati Amber Rose akiwa na miaka 32.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, mrembo huyo ameiweka picha yake akiwa na kijana huyo anayejulikana kwa jina la Terrence Ross, anayechezea timu ya Toronto Raptors.
Uhusiano wa wawili hao inasemekana ulianza tangu siku ya wapendanao (Valentine day) mwaka huu walipokutana katika mchezo wa kikapu wa NBA All-Star game.
“Ni wazi kwamba nimemalizana na wasanii wa muziki na sasa nimepata sehemu sahihi na ni tofauti,” aliandika Amber Rose, baada ya kumpata mpenzi wake huyo mpya.