Sharapova ambaye ni raia wa nchini Urusi, mwenye umri wa miaka 28, amepimwa na kubainika kutumia dawa aina ya Meldonium, ambazo amekua akitumia toka mwaka 2006.
Mcheza tenisi huyu mshindi wa Grand Slam mara tano, alisema hakujua vikwazo atakavyokuja kukutana navyo baadaye.
“Kwa miaka 10 nimekua nikitumia dawa zinazoitwa Mildronate nikipewa na daktari wangu na familia yangu.
“Siku chache zilizopita nilipokea barua kutoka kwa Shirikisho la Tenisi la Kimataifa (ITF), juu ya dawa hizo na nikagundua kuwa zina jina jingine la Meldonium.
“Ni muhimu sana kuelewa kwa miaka 10 dawa hizo hazikua kwenye orodha ya shirika la kudhibiti matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni (Wada), lakini sheria zilibadilika January na kuzifanya dawa za Meldonium kukatazwa, kitu ambacho sikufahamu. Desemba mwaka jana nilipata barua pepe toka Wada kuhusu mabadiliko kwa dawa zilizokatazwa, ila sikufungua barua hiyo na ndiyo maana yamenikuta haya,” alisema Sharapova.