22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Madaftari ya 2pac yaokotwa

2pacLAS VEGAS, MAREKANI

KATIKA hali ya kushangaza madaftari aliyokuwa akiandikia mashairi ya nyimbo zake mkali wa zamani katika muziki wa hip hop nchini Marekani, Tupac Shakur ‘2pac’ ambaye amefariki dunia Septemba 13, 1996 yamepatikana.

Madaftari hayo yalikutwa pamoja na CD tatu zenye nyimbo zake ambazo bado hazijatambulishwa kwenye vyombo vya habari.

Vitu hivyo vimeokotwa kwenye mabegi yake yaliyokuwa kwa mama yake Afeni, jijini Carolina, ambapo madaftari mawili yalikuwa yamejaa mashairi yaliyoyaandikwa kwa mkono.

Daftari moja lilikutwa likiwa limeandikwa mipango juu ya video zake jinsi anavyotaka ziwe baada ya kurekodi. Hata hivyo, mama huyo amepanga kuuza kumbukumbu hizo ingawa baadhi ya ndugu zake wanataka kazi hizo ziifadhiwe na kuwa kumbukumbu kwa kizazi kijacho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles