26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

AMBER ROSE, 21 SAVAGE WAACHANA

LOS ANGELES, MAREKANI


MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Amber Rose, ametumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza kuachana na mpenzi wake rapa, Shayaa Bin Abraham maarufu kwa jina la 21 Savage.

Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha mwaka mmoja, hivyo mrembo huyo ameweka wazi kuachana kwao.

“Nadhani mara ya mwisho kuonekana na 21 Savage ilikuwa siku ya wapendanao, lakini kwa sasa kila mmoja anafanya mambo yake.

“Kuna kipindi nilikuwa na furaha ya mapenzi, lakini sasa nataka kupambana na kazi zangu bila ya kujihusisha na uhusiano,” aliandika Amber Rose.

Kila mmoja kati ya wawili hao ameamua kuondokana na mwenzake kwenye akaunti yake ya Instagram, hivyo inamaanisha hawapo pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles