23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

NONDO KUFIKISHWA MAHAKAMANI WAKATI WOWOTE

Na Leonard Mang’oha, Dar es Salaam

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote.

Amesema mwanafunzi huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika na kuongeza kuwa bado anaendelea kushikiliwa polisi kwa upelelezi zaidi kutokana na makosa aliyofanya.

Kamanda Mambosasa amesema hayo leo Ijumaa Machi 16, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu kuendelea kushikiliwa kwa mwanafunzi huyo muda mrefu bila kufikishwa mahakamani.

‘‘Anashikiliwa kwa sababu ametenda makosa na wewe hujashikiliwa kwa sababu huna makosa kama unataka kufahamu kwa nini anashikiliwa tenda kosa hata umvamie mtu umtwange makofi, ni lazima utashikiliwa,’’ amesema Mambosasa.

Kuhusu taarifa za mawakili wa Nondo kunyimwa nafasi ya kumwona Mambosasa alisema hakuna aliyenyimwa nafasi ya kufanya hivyo kwa sababu hakuna aliyefika ofisini kwake kuomba kumwona akazuiwa.

‘‘Kama mtu anakuja anaishia kwa askari huko chini wanamzuia naye anakubali anaondoka, anakuwa hajaamua kuja kumwona, kwa sababu pamoja na kushikiliwa ana haki ya kuhudumiwa na kupewa matibabu kama binadamu kwa sababu ni haki yake,’’ amesema Mambosasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles