Alonso apongeza falsafa ya Guardiola

0
673

downloadMunich,Ujeruman

KIUNGO wa Bayern Munich Xabi Alonso ameipongeza falsafa ya soka ya kocha anayetarajiwa kuondoka Bayern Pep Guardiola  kwa kuamini  kuwa msingi thabiti alioutengeneza  katikma timu hiyo  utadumu kwa muda mrefu hata baada ya kuondoka kwake.

Kocha huyo wa Kihispania ameanza kampeni nyingine ya kuwa mtawala katika soka huku mataji matatu yakiwa ndani ya uwezo wake msimu huu, lakini atatimkia Uingereza kuchukua kibarua cha Manchester City majira ya joto.

Baadhi ya mashabiki wa Bayern waliukosoa mfumo wa kocha huyo ambao umeegemea katika kumiliki mpira lakini Alonso amesema kikosi kizima sasa kinakubaliana na maono ya Guardiola.

“Inaweza isiwe rahisi kukwambia, kwa sababu Pep yupo mbele ya wakati. Kocha huyo anahitaji mafanikio yake binafsi na ya wachezaji pia,,”  alisema Alonso.

“Lakini mara utakapoelewa, kama kwa upande wangu hivyo ndivyo tunavyopenda kucheza. Tunapenda kucheza kwa kumiliki zaidi, naye anapenda hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here