27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Mtibwa kuivaa Mwadui kwa tahadhari

MTIBWA SUGARNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar imejipanga kucheza kwa tahadhari kubwa ugenini itakapovaana na Mwadui FC katika mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayopigwa Uwanja wa Mwadui, Shinyanga.

Katika mchezo wa awali uliofanyika Uwanja wa Manungu, Morogoro, Mwadui iliambulia kipigo kikali cha mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Thobias Kifaru, alisema anaamini Mwadui watakuwa wamejiandaa kulipiza kisasi watakapokutana Aprili 3, mwaka huu, lakini wamejipanga vyema kuhakikisha wanaendeleza kipigo kwa wapinzani wao.

“Tulipoteza mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar, hivyo hatuwezi kuruhusu kufungwa mara ya pili mfululizo, ni lazima tucheze kwa umakini wa hali ya juu tutakapocheza na Mwadui,” alisema.

Kifaru alisema wanaendelea kupambana ili kuhakikisha wanamaliza michuano ya Ligi Kuu Bara msimu huu wakiwa nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

Kwa sasa Mtibwa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha pointi 39, sawa na maafande wa Tanzania Prisons, lakini wakitofautiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles