27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

AKOTHEE AMPA ZAWADI YA GARI BINTI YAKE

NAIROBI, KENYA


STAA wa muziki nchini Kenya ambaye anatamani kuwa na watoto wengi zaidi, Esther Akoth ‘Akothee’, amempa zawadi ya gari Mazda CX-7 mtoto wake wa pili, Rue maarufu kwa jina la Celine Dion baada ya kutimiza miaka 19.

Msanii huyo alimpa binti yake zawadi hiyo yenye thamani ya zaidi ya milioni 22, huku akimtaka kukataa zawadi na lifti kutoka kwa wanaume wakware.

“Chukua funguo, nina uhakika unaweza kujigharamia mafuta na matengenezo madogo madogo kutokana na mshahara ninaokulipa unaotokana na matunzo na malezi mazuri unayowapa wadogo zako, tafadhali epuka zawadi kutoka kwa wanaume, epuka vinywaji na lifti za bure.

“Hakuna mwanamume atakayekupa kitu bure, wakikupa ujue kuna siku watafuata malipo, kuwa mwenye mawazo huru sasa umepata usafiri wa kwenda nao shule, asante kwa kuwa binti mwema nakupenda,” aliandika Akothee kwa binti yake.

Binti yake alipopata ujumbe huo naye akajibu: “Nilipoona hali hiyo sikuweza kujieleza kwa mshtuko…mama utabaki kuwa mama mwema, nitalipenda gari langu muda wote na pia sitapokea zawadi wala lifti kwa kuwa nina la kwangu, nakupenda mama.”

Licha ya kutoa zawadi hiyo ya gari, zaidi ya Sh milioni 10 zilitumika katika sherehe hiyo ya binti huyo iliyofanyika Mombasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles