29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

AJALI YAJERUHI 25 WA FAMILIA MOJA MOROGORO

Na Ramadhan Libenanga

-Morogoro

WATU 25 wa familia moja wamejeruhiwa katika ajali baada ya lori kugongana na basi walilokuwa wakisaifiria.

Ajali hiyo ilitokea jana wilayani Mvomero ambako basi hilo lililogongana na lori  namba T 712 CHQ Scania likiwa na tela  namba  T 591 BYS ambalo lilikuwa likijaribu kuyapita magari mengine.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei, alisema baada ya lori  hilo kushindwa kuyapita magari hayo, liligonga basi la Karim Trans   namba za usajili T 465 DGQ.

Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Mathew Benedict,   likitokea Turiani wilayani Mvomero kwenda mjini Morogoro.

Lilikuwa limekodiwa na familia ya Matesa  ambayo ilikuwa ikienda kumaliza msiba wa baba yao.

Kamanda Ulrich alisema majeruhi wengine walitibiwa na kuruhusiwa  huku 25 wakilazwa katika Hospitali ya Rufaa Morogoro kwa matibabu zaidi .

“Tumepokea majeruhi wengi lakini wengi wao hawajaumia sana na wametibiwa na kuruhusiwa,” alisema Kamanda Matei

Aliwataja baadhi ya majeruhi walioumia katika ajali hiyo kuwa ni Odilia Ipoliti, Zainabu Mahamba, Shukuru Mrisho, Sauda na Anna ambao wametambulika kwa jina moja.

Kamanda Matei alisema   chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori ambaye alikuwa akijaribu kuyapita magari mengi kwa pamoja na kusababisha ajali hiyo.

“Tunashukuru Mungu hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hii.

“Na tunawaomba madereva wote kuwa makini hasa wanapokuwa barabarani  wanapoendesha vyombo vya moto,” alisema Kamanda Matei.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles