25.5 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Afya yamzuia Pele kutoka ndani

Rio de Janeiro, Brazil

GWIJI wa zamani wa soka nchini Brazil, Edson do Nascimento maarufu kwa jina la Pele, ameripotiwa kuwa, hataki kutoka nje ya nyumba yake kutokana na matatizo ya afya yake.

Mtoto wa nyota huyo wa soka Edinho, amedai kuwa anaona aibu kwa jinsi alivyo, hivyo ameweka wazi kuwa kutokana na hali hiyo hawezi kutoka nje.

Pele mwenye umri wa miaka 79, anatarajia kutimiza miaka 80 Oktoba mwaka huu, lakini afya yake inamfanya atembee kwa kutumia kiti cha wagonjwa kwa miaka kadhaa kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya nyonga.

“Kwa sasa yeye ni dhaifu, alipandikizwa nyonga ila hali yake bado haijakaa sawa jambo ambalo linamfanya awe anakaa ndani. Ili sio tatizo la leo, limekuwa kwa muda mrefu.

“Yeye ni staa hapa duniani, hivyo anatamani kuonekana mitanaani mbele ya mashabiki zake, lakini hana furaha kukutana na mashabiki huku akiwa kwenye kiti cha wagonjwa, lakini ninaamini kama angekuwa anaweza kutembea vizuri basi angeweza kutoka nje bila ya msaada wowote.

“Ukweli ni kwamba Pele ana aibu sana, ila tunashukuru kuona hali yake inabadilika taratibu huku akijaribu kutembea, lakini bado hayupo sawa,” alisema mtoto wa mchezaji huyo.

Pele kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni alikuwa anasumbuliwa na tatizo la figo na aliripotiwa kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kulitoa jiwe kabla ya kuibadilisha moja kwa moja.

Pele mara ya mwisho kuonekana mbele za watu wengi ilikuwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, lakini mwezi mmoja baada ya kumalizika kwa michuano hiyo alizidiwa na kukimbizwa hospitalini. Mbali na mchezaji huyo kusumbuliwa na nyonga, lakini alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kibofu cha mkojo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles