31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Afrika Kusini yaipiku Nigeria kiuchumi

randNEW YORK, MAREKANI

AFRIKA Kusini imerudisha hadhi yake ya miaka mingi kama taifa lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika baada ya kuipiku Nigeria.

Nigeria, ilitwaa hadhi hiyo kipindi cha miaka miwili iliyopita kufuatia kukua kwa sekta nyingine za uchumi mbali ya nishati ya mafuta, ambayo ndiyo inayoubeba uchumi wa taifa hilo.

Mwelekeo huo unatokana na ukukotoaji wa mapato ya ndani ya mataifa hayo mawili uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) mwaka jana.

Kipindi cha mwaka huu, sarafu ya Afrika Kusini, Rand na Naira ya Nigeria zimeshuhudia zikichukua mwelekeo kinzani dhidi ya dola ya Marekani.

Rand ilishuhudia ikiimarika dhidi ya dola ikipanda kwa asilimia 16 huku Naira ikipoteza theluthi moja ya thamani yake.

Hata hivyo, hali hiyo ya Afrika Kusini kiuchumi inaweza kupanguliwa tena kutokana na pato lake la ndani la dola bilioni 301 kuizidi Nigeria kwa dola bilioni tano tu.

Chumi zote hizo ziko katika hatari ya kuporomoka kwa sababu mbalimbali ikiwamo udhaifu wa udhibiti, kushuka kwa bei ya mafuta huku zikiwa zimeyumba katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles