29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

AFCFTA wakubaliana baadhi ya vigezo vya uasilu wa bidhaa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, ameshiriki mkutano wa 7 wa Baraza la Mawaziri wa Afrika wanaosimamia Biashara wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) uliofanyika kwa njia ya kawaida na mtandao (hybrid)  Oktoba 10, 2021)  ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba.
 
Mawaziri hao walipitia hatua iliyofikiwa katika masuala mbalimbali yaliyomo katika Awamu ya Kwanza ya Majadiliano, ambayo bado hayajakamilika na kufanya maamuzi.

Aidha, wametoa muda wa miezi mitatu kwa wataalam kukamilisha maeneo ambayo hayajakamilika ili kukamilisha majadiliano hayo kwa asilimia 100
 
Aidha Mawaziri hao walikubaliana baadhi ya vigezo vya uasili wa bidhaa na kufanya vifikie asilimia 88.1 kutoka asilimia 86.03 ya awali ikiwemo vigezo vya uasili wa bidhaa za Maziwa (cheese and curd), Juisi za matunda (Cranberry juice, mixture of juices), na vifaa vya bidhaa za ngozi (Articles of leather).
 
Tanzania imeridhia Mkataba wa AfCFTA ambao hadi sasa jumla ya nchi 38 kati ya nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika zimeridhia Mkataba huo huo ulianza kutekelezwa rasmi Mei 30, 2020.

Jumla ya nchi 41 zimewasilisha mapendekezo ya tariff offer kwa ajili ya kuanza kufanya biashara. Kati ya nchi hizo, zipo jumuiya nne (4) za Umoja wa Forodha ambazo ni Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC), Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (CEMAC), Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Umoja wa Forodha Kusini mwa Afrika (SACU).  
 
Prof. Mkumbo amesema Tanzania inatarajia kunufaika na kutumia fursa zote za kibiashara zinazotokana na Makataba huo ikiwemo kupatikana kwa masoko mapya ya mazao ya kilimo yatakayochochea uzalishaji, kuimarika kwa mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo yanayohusisha wakulima wadogo kama vile alizeti, pamba, karafuu, viungo, matunda na mbogamboga kutokana na kuongezeka kwa soko la bidhaa zitakazozalishwa nchini
 
“Pia kuna kuongezeka kwa uzalishaji na ajira kwa wakulima na wadau wanaohusika katika mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo, kupatikana kwa soko kubwa la bidhaa na huduma lenye idadi ya watu takriban bilioni 1.2 ukilinganisha na idadi ya watu takribani milioni 522 katika nchi za EAC na SADC.

“Kuongezeka kwa tija na ubora kwa bidhaa na huduma za Tanzania kutokana na kuongeza kwa ushindani na hivyo kupelekea kupungua kwa bei za bidhaa,”amesema Prof. Mkumbo na kuongeza kuwa:

“Faida nyingine za kuridhia mkataba huo ni pamoja na na Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara sambamba na kuviendeleza viwanda na wajasiriamali kundi la Wajasiriamali wodogo sana, Wadogo na wa Kati (MSMEs), Upatikanaji wa bidhaa za aina mbalimbali (varieties) nchini na Uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje ya nchi (technology transfer) kutokana na uwekezaji utakaofanyika nchini,” amesema Prof. Mkumbo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles