28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yasherehekea miaka 6 ya utoaji huduma na watoto (MOI)

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya Simu ya Halotel na Wafanyakazi wake, leo wamewatembelea watoto wenye changamoto ya Kiafya Vichwa Vikubwa na Mgongowazi pamoja na Wazazi waliolazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Mhimbili (MOI) kwa ajiri ya kusherehekea pamoja nao katika kuahamisha miaka 6 ya Kampuni hiyo na Utoaji wa huduma za Mawasiliano na ikiwa ni pamoja na kuwaletea Mahitaji mbalimbali ya Kijamii kama sehemu ya msaada wao kama wafanyakazi.

Mahitaji hayo ambayo ni pamoja na dawa na Mahitaji mhimu ya kibinadamu ambayo yatawawesesha watoto hao kuimarisha afya zao pindi wawapo wodini wakisubiri kupatiwa matibabu ambayo ni kwa njia ya upasuaji .

Akizungumza wakati wa kukabodhi Mahitaji hayo leo Jumanne Oktoba 12, Mkuu wa Kitengo cha bidhaa na mawasiliano, Sakina Makabu, pamoja na Afisa Mahusiano ya nje ya Halotel, Yassir Matsawily, amesema kuwa katika kuhakikisha wanasaidia sekta ya afya nchini ni vyema kuendekeza fursa hii ya kuja kuwaona watoto hawa na kusherehekea pamoja na kuwapa msaada ili waweze kuimarika kiafya wanapoendelea kupata matibabu wodini hapa ikiwa ni kuobyesha upendo kwao na kutambua thamani yao katika jamii ya Watanzania.

“Tunatambua changoto mabalimbali ambazo ziko katika kuwapa matibabu watoto wenye matatzo ya kiafya ya vichwa vikubwa na mgongowazi wawapo wodini wakisubiri kupatiwa matibabu ya upasuaji hivyo katika kujali na kutambua thamani ya Afya zao tumeona ni vema kuwaletea mahitaji haya mhimu ya kuimarisha afya zao, aliongeza Yassir,”amesema.

Akiongea baada ya kukabidhiwa msaada huo kwa niaba ya W=wazazi wengine wodini hapo, Rose Vincent, amesema kuwa wanajisikia faraja kukumbukwa na Kampuni hiyo na kupokea msaada huo kutoka kwao .

“Tumefarijika sana na tunaomba waendelee na moyo huo huo wa kusaidia jamii ya Watanzania,” alisema Vincent.

Kwa upande wa uongozi wa Taasisi ya Tiba na Mifupa (MOI) , Afisa uhusiano Patrick Mvungi, amesema kuwa ni faraja kupokea msaada huu kutoka kampuni ya simu ya Halotel na Wafanyakazi wake, na kutjamini Afya za watoto Hawa , lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kunisaidia sekta ya afya nchini.

“Hii ni hatua mpya na kubwa na imekuwa endelevu kwetu sisi katika kuimarisha ushirikiano wwtu na Halotel kwa kiwango cha juu hasa katika kuboresha sekata ya afya kwa ujumla,” alisema Mvungi.

Licha ya Kampuni ya Halotel kupiga hatua kubwa katika kusambaza huduma za Mawasiliano na kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu nchi nzima, kampuni hii imekuwa imekuwa ikijihusisha na kujali jamii ya Watanzania kwa nyanja mbalimbali ikiwamo kuboresha sekta ya afya na elimu kama moja ya kipaumbele cha kampuni ya hii kwa maendeleo ya Watanzania na nchi nzima kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles