28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Adaora Music, mwimbaji Mmarekani aiweka wazi ‘Chain Breaker’

Maryland, Marekani

KAMA ulidhani mwimbaji wa Injili, Adaora Music alikuwa amemaliza basi umekosea kwani ndio kwanza ameachia ngoma yake mpya inayokonga nyoyo za wapenzi wa muziki huo.

Wakati akitamba na wimbo wake ‘I Can’ aliomshirikisha Papa San au ule ‘I Come’ au ‘My African Praise Remix’ alioshirikiana na Peter Tone sasa ameachia wimbo mpya unaoitwa Chain Breaker.

Adaora anasema kwenye wimbo wa Chain Breaker aliomshirikisha Moses Bliss na kutayarishwa na Peter Tone umejaa upako na mguso wa kipekee kutokana na vionjo vya muziki wa Injili wa kisasa.

“Wimbo huu unatukumbusha kwamba sisi ni washindi kwa sababu Yesu amevunja kila mnyororo hivyo naomba mashabiki wa gospel kufurahia wimbo huu wa hamasa ulioandikwa na mimi mwenyewe Adaora,” amesema mwimbaji huyo.

Adaora Music ni mwimbaji wa nyimbo za hamasa kwenye kizazi hiki na mtunzi mzuri huko Maryland nchini Marekani akiwa na asili ya Nigeria na muziki wake umejaa uasili wa tamaduni za makabila mbalimbali.

Mwimbaji huyo tayari ametoa nyimbo kadhaa na kupitia muziki wake, Adaora amefanikiwa kuunda mtandao mkubwa wa watu wakiwemo wanawake, makundi maalumu na kushirikiana na mashirika mbalimbali huku akionekana kwenye vipindi vya runinga kubwa nchini Marekani.

Aidha Adaora ni mtaalam na veterani wa Jeshi la Anga nchini Marekani ana PhD ya kemia ya dawa, na sasa anafanya kazi ya kuboresha programu za matibabu za Jeshi.

Adaora ni kiongozi wa kusifu na kuabudu pia ni mshauri wa Huduma ya Vijana na Watu Mashuhuri (YASM) huko Mercy Seat Chapel, RCCG, Gaithersburg Maryland.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles