24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kuwavuta Watalii Tanzania

Na MWANDISHI WETU

KLABU ya Yanga imeingia makubaliano ya kutangaza Utalii wa Tanzania kupitia mlima Kilimanjaro pamoja na Visiwa vya Zanzibar kwa kuweka nembo ya  iliyoandikwa visit  Kilimanjaro & Zanzibar  katika jezi zake

Hatua hiyo inakwenda sambamba na juhudi za  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii wa nchi kupitia kipindi maarufu cha Royal Tour alichokianzisha yeye mwenyewe.

Akizungumza leo Septemba 17, jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro, ameipongeza Yanga kwa  kuleta wazo hilo la kuutangaza utalii wa Taifa, kupitia safari zake za Kimataifa katika mchezo wake wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United  ya Nigeria na michezo mingine kama itafanikiwa kufuzu raundi inayofuata.

“Timu ya Yanga imeweka nembo ya Mlima Kilimanjaro, visiwa vya Zanzibar katika Jezi zao zote, ili kutangaza utalii wa Tanzania bure kabisa bila hata malipo, lakini kama wangetaka pesa basi ingekuwa zaidi ya bilioni 1 za Kitanzania kuweka nembo hii kwenye jezi hizo,” amesema Dk. Ndumbaro.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga,  Haji Mfikirwa, amesema klabu hiyo inafanya hayo yote kuunga mkono jitihada za Tanzania kuendelea kutangaza utalii wake, na kwamba hiyo ni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mashabiki ndani na nje ya nchi kitendo kinachoweza kuvutia idadi kubwa ya watalii duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles