32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

CDF Trophy yapamba moto Lugalo

NA WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

Mashindano ya wazi ya gofu,CDF Trophy yameanza rasmi  leo  Septemba 17,2021 kwenye viwanja vya Klabu ya Lugalo jijini Dar es Salaam, huku mchezaji Frank Mwinuka  wa Lugalo akiongoza  siku ya kwanza kwa mikwaju 67.

Michuano hiyo ambayo imeanza na wachezaji wa kulipwa, (proffesionals),  Mwinuka ameshika namba moja akifuatiwa na  Hassan Kadio wa Dar es Salaam Gymkhana  aliyefungana na Abdallah Yusuph kwa mikwaju 73 huku wa tatu akiwa ni  Rajabu Pembe aliyechapa mikwaju 75.

Akizungumzia mashindano hayo, Mwinuka amesema  anafurahi kuongoza kwa siku ya leo na wanatarajia kuendelea Jumapili katika hatua ya fainali.

Naye Kadio amesema kuwa: “Mchezo sio mbaya nimecheza kiasi fulani vizuri inangawa tumefungana wawili na Abdallah Yusufu wa Lugalo na yupo anayeongoza wa hapa hapa Lugalo amecheza vizuri,”

Kwa upande wake Abdallah Yusuf ambaye pia ni mwalimu wa mchezo huo, amesema hawezi kuahidi ushindi bali anasubiri siku ya mwisho  ya kufunga mashindano.

Mashindano hayo ambayo yanashirikisha wachezaji wa ridhaa zaidi ya 100 wanaotarajia kucheza kesho, yatafikia tamati  Jumapili Septemba 19 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles