32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi yatoa tamko kesi ya Mbowe

Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Tanzania limetoa taarifa za awali za uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe lililotokea wakati kiongozi huyo alipovamiwa wakati akiwa anapanda ngazi kuingia nyumbani kwake eneo la Medel jijini Dodoma.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, David Misime leo Ijumaa Juni 12, akitoa taarifa hiyo ya uchunguzi wa awali amesema kulingana na upelelezi walioufanya wamebaini kuwa maelezo aliyoyatoa kiongozi huyo na dereva wake yanatia mashaka.

Misime amesema kwa mujibu wa mashahidi waliokuwa katika eneo la la tukio hakuna hata mmoja aliyesikia kelele za kuomba msaada au kuona Mbowe akishambuliwa.

Amesema Jeshi la Polisi linaendela kufanya upelelezi wa kina kuanzia kwa Mbowe ambaye alidai kuwa muda wa saa saba usiku akiwa kwenye ngazi ya kuingia nyumbani kwake akiwa anatokea kwa mzazi mwenzake, Joyce Mukya, alishambuliwa na kuumia mguu wa kulia.

“Mhanga wa tukio anadai wakati anashambuliwa alipiga kelele nyingi kuomba msaada ambao aliupata kutoka kwa dereva wake ambaye naye alipiga simu kwa Joyce Nkya kumjulisha tukio hilo na hatimaye wakaamua kuondoka kwenda kwa Joyce kisha hospitali iliyoko takribani kilomita tano nje ya jiji la Dodoma pasipo kuona umuhimu wa kutoa taarifa polisi.

“Ushahidi pekee unaozungumzia kushambuliwa ni maelezo ya mhanga wa tukio pamoja na dereva wake ambavyo kwa hali ilivyo sasa yanatia shaka kuhusu ukweli wa tukio hili.

“Mashaka hayo yanaongezeka zaidi pale tulipobaini kuwa nyumbani kwa Mbowe alikuwepo kijana wake, James Mbowe ambaye hawakuona umuhimu wa kumjulisha kuhusu tukio lililotokea hapo nyumbani badala yake wakaona umuhimu wa kumjulisha Joyce Mukya aliyekuwa mbali na tukio,” amesema Misime.

Amesema kuwa uchunguzi wao umethibitisha kuwa Juni 6 mwaka huu Mbowe aliembelea sehemu kadhaa za starehe zinazouza vileo na kupata kinywaji na kwamba hata alipofika hospitalini alionekana akiwa katika hali ya ulevi kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles