24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu Amos afikishwa Mahakamani kwa uhujumu uchumi

Derik Milton, Simiyu

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu jana imemfikisha mahakamani katibu wa Chama cha msingi cha Ushirika cha Mwanga kituo cha Nangale Wilayani humo Masanja Mbula kwa kesi ya uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo jana kwa waandishi wa habari, Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na makosa manne ikiwemo wizi, kughushi nyaraka, kuisababishia harasa Amcos na Uhujumu uchumi.

Taarifa hiyo ya Takukuru imesema kuwa Mtuhumiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Simiyu na kusomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Amani Mohamed mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Venance Mlingi.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kughushi nyaraka na kujipatia kiasi cha sh. 7,000,000, kosa jingine ni wizi wa sh. Milioni 12,000,000, kuisababishia hasara mamlaka kiasi cha sh. 22, 584,350 ambapo kesi yake ni namba 23/2020 uhujumu uchumi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mtuhumiwa huyo alipokea kiasi cha sh. Milioni 221,000,000 kutoka Kampuni ya NGS Investement Co. Ltd ili akawalipe wakulima lakini hakufanya hivyo na kuamua kutoweka nazo.

Aidha taakukuru wameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alianza kusakwa, ambapo alikamatwa akiwa machimboni Mkoani Singida na kusafirisha kurudishwa Simiyu kwa ajili ya kufikishwa mahakani.

Mtuhumiwa alirudshwa rumande kutokana na kesi yake kutokuwa na dhamana, ambapo hakimu alihairisha hadi juni 24 kwa ajili ya kutajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles