23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwinuka amtaka mkandarasi kuongeza kasi ujenzi Ofisi za TANESCO Geita

Mwandishi Wetu, Geita

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dk. Tito Mwinuka na Menejimenti ya TANESCO wametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya ofisi za TANESCO Mkoa wa Geita pamoja na Wilaya ya Chato, ujenzi unaotekelezwa na Wakala wa Majengo (TBA).

Dk. Mwinuka amesema kuwa ujenzi wa majengo hayo ni sehemu ya jitihada za shirika kuhakikisha linaendesha shughuli zake katika majengo yake na hivyo kuepukana na gharama kubwa za upangishaji majengo kwa matumizi za ofisi za Shirika kuanzia ngazi za Kanda, Mkoa mpaka Wilayani.

Aidha Dk. Mwinuka ameongeza kuwa lengo hilo linakwenda sambamba na maagizo ya Serikali ya kuhakikisha kuwa ofisi zote za Serikali na umma zinajenga na kumiliki majengo ya ofisi zake katika maeneo yote ambapo zinaendesha shughuli zake.

‘’Leo hii nimetembelea kukagua na kujionea ujenzi unaoendelea wa majengo ya ofisi za TANESCO, Mkoa wa Geita na Wilaya ya Chato, ambapo yote ujenzi wake unakwenda vizuri chini ya Mkandarasi TBA akiwa chini ya usimamizi wa Karibu wa TANESCO, niwaagize kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha majengo haya mapema zaidi ili Shirika liweze kuondokana na matumizi ya nyumba za kupanga kama ofisi na kuhamia katika majengo yake”, amesema Dk. Mwinuka

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Godfrey Mwakabole alieleza ujenzi unakwenda vizuri na kwa kasi inayoridhisha na matatajio yaliyopo ni kumaliza majengo yote mawili ndani ya Mwezi Agosti 2020 ili TANESCO iweze kuhamia katika majengo hayo tayari kwa kuendelea na shughuli zake.

Aidha kwa upande wa TANESCO Mkoa wa Geita Meneja wa mkoa huo, Mhandisi Joachim Ruweta aliishukuru Menejimenti ya Shirika kwa ushirikiano mkubwa amabo imekuwa ikiutoa katika kuharakisha shughuli za ujenzi wa majengo hayo na kueleza kuwa kukamilika mapema kwa majengo hayo itakuwa ni moja ya hatua kubwa katika uboreshaji wa huduma za umeme na mazingira ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wa ofisi husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles