26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

TCRA waja na tuzo za Tehama

Leonard Mang’oa -Dar es salaam

MAMLAKA ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuweka mikakati ya kuboresha ushiriki wa vyombo hivyo katika tuzo za tehama zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Akizungumza katika mkutano na wahariri hao Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba, alisema kuwa mamlaka hiyo ingependa kushirikiana zaidi na vyombo vya habari kwa kuzingatia mkataba wa huduma kwa mteja unaozihusisha pande hizo mbili.

Kilaba alisema kuwa mkataba huo umekusudia zaidi kuimarisha utamaduni wa utendaji bora unaozingatia mahitaji, matakwa na matarajio ya wateja na wananchi kwa ujumla.

“Aidha, kwa mkataba huo tumejitanabaisha kujali zaidi mteja wa TCRA. Ningependa kutoa rai kwenu kushirikiana katika tukio la tuzo hizi ambalo ninyi ni sehemu kamili ya wadau wa mawasiliano.

“Mimi binafsi ninaelewa na ninathamini nguvu ya vyombo vya habari katika kuelimisha na kuhabarisha umma. Hatua tuliyofikia katika utaratibu huu wa tuzo za tehama, inahitaji uhamasishaji wenu kwa kuhimiza kila mmoja wenu kushiriki, lakini kuwaelimisha wengine kushiriki pia,” alisema Kilaba.

Alisema tuzo hizo zinalenga kuwatambua na kuwatunuku watoaji wa huduma bora zaidi za mawasiliano, kuongeza ubunifu katika utoaji wa huduma za utangazaji, kuongeza ubora na ufanisi wa huduma za mawasiliano katika sekta ya posta, simu, utangazaji na intaneti pamoja na kuongeza chachu na mchango wa sekta ya mawasiliano katika kukuza uchumi wa kidigitali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles