27.6 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Watangazaji wa Clouds wapandishwa kizimbani

NA KULWA MZEE- DAR ES SALAAM 

MTANGAZAJI wa Clouds kipindi cha Shilawadu, Soud Kadio (Soud Brown) na wenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakishtakiwa  kutumia maudhui mtandaoni bila kuwa na kibali.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani jana na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nguka akishirikiana na wakili Estazia Wilson.

Mshtakiwa Soud alisomewa mashtaka  mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi., Augustino Rwizile.

Wakili Nguka alidai kati ya Juni 11 na Septemba mwaka huu Dar es Salaam kwa kutumia online TV inayojulikana kwa jina la Shilawadu TV,  kinyume cha sheria, Soud alitoa maudhui katika mtandao huo bila   kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mshtakiwa huyo alikana shitaka hilo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala aliomba mteja wake huyo apewe dhamana kwa sababu shtaka linadhaminika.

Hakimu Rwizile alikubali kumpa dhamana mshtakiwa kwa masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni mbili,  na mshtakiwa mwenyewe asaini dhamana ya kiasi hicho cha fedha.

Mshtakiwa Soud alikamilisha masharti ya dhamana na kuachiwa huru na kesi iliahirishwa hadi Oktoba 18 mwaka huu itakapotajwa tena.

Wakati huo huo, washtakiwa  wawili Shafii Dauda na Benedict Kadege,  wamefikishwa katika Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,  Kelvin Mhina wakituhumiwa kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka akishirikiana na mawakili Mutalemwa Kishenyi na Mwanaamina Kombakono, walidai makosa hayo yanadaiwa kufanyika  kati ya Juni na Septemba mwaka huu.

Kombakono alidai   kati ya Juni 14 hadi Septemba mwaka huu ndani ya Dar es Salaam, kwa kutumia online TV inayojulikana kwa jina la Shafii Dauda,  kinyume cha , walitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka TCRA.

Washtakiwa waliachiwa kwa  dhamana na kesi imeahirishwa hadi Oktoba 8 mwaka huu itakapotajwa tena.

Katika hatua nyingine Wakili wa Serikali Mkuu, Tumain Kweka alimsomea mashtaka  MC Luvanda akidai alitumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania.

Alidai kati ya February 24 na Septemba 2018 Dar es Salaam,  Mc Luvanda alianzisha na kutumia mtandao wa  www.mcluvanda.com ambao haukuwa na kikoa cha .tz.

Mc Luvanda anadaiwa kuwa katika kipindi hicho  alitoa huduma hiyo kupitia online TV  inayofahamika kama MC Luvanda bila  kibali kutoka TCRA.

Mshtakiwa aliachiwa kwa dhama na kesi iliahirishwa hadi    Oktoba 23 mwaka huu itakapotajwa tena.

Naye Mpigapicha Michael Mlingwa alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akituhumiwa kutumia mtandao bila usajili.

Akisoma mashtaka, Faraja Nguka, alidai  Februari 24 mwaka huu jijini Dar es Salaam kinyume cha sheria, mshitakiwa alikutwa  anamiliki na kutumia mtandao wa WWW.Slidevisual. Com bila leseni kutoka TCRA.

Mshtakiwa alikana mashtaka na yuko nje kwa dhamana  hadi Oktoba 8 kesi itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles